Daily Archives: June 14, 2012

TANGAZO LA MUHADHARA KWARARA


BISMILLAH RAHMANI RAHIM

ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH

WAISLAMU WOTE WA MJINI NA MASHAMBA KIKE NA KIUME MNATANGAZIWA KUHUDHURIA KWENYE MUHADHARA UTAKAOFANYIKA KWARARA MASJID TAALIM KWA BATASHI SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 16JUN2012 UTAANZA BAADA YA SWALATU ASIR. MUISLAMU USIKOSE UKUMBUSHO HUU WA KHEIR, NI MUHIMU KWA AJILI YA DINI NA DUNIYA YAKO.

WABILLAH TAUFIQ

Advertisements

Muelekeo kuelekea ukombozi wa Zanzibar


Amir Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu, Sheikh Msellem Ally Msellem (aliyesimama), akizungumza katika moja ya mihadhara yake mjini Zanzibar

Jumuiya ya Uamsho inafanya kazi hiyo kwa kushirikiana kikamilifu na jumuiya na taasisi tafauti za Kiislamu nchini Zanzibar kwa  kutetea maslahi ya kupatikana kwa mamlaka kamili ya Serikali ya Zanzibar kutokana na kushindwa kwa vyama vya siasa kutetea Utaifa wa Zanzibar, kwa sababu vyama hivyo vimezingirwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo kimsingi hairuhusu kuzungumza lolote kuhusu Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.” Read the rest of this entry