Monthly Archives: June 2012

TAARIFA MAALUM KWA VYOMBO VYA DOLA

MSIMAMO WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISILAMU ZANZIBAR JUU YA MCHAKATO WA KATIBA


JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI-ZANZIBAR
24/06/2012

Bismillahir Rahmaanir Rahiim
Kila sifa njema zinamstahikia Allah (S.W.T), rehema na amani zimuendee Mtume wake, ahli zake na wafuasi wake wote waliomfuata kwa wema. Baada ya vikao tofauti vya uongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Zanzibar, zimeonelea kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki katika mchakato wa kutoa maoni kuhusu katiba mpya kwa sababu kuu zifuatazo: Read the rest of this entry

TAMKO LA TAASISI ZA KIISLAMU KUHUSU KUVUNJWA KWA MUHADHARA DONGE


19 JUN, 2012

 BISMILLAH RAHMANI RAHIM

TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W.T), Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), watu wake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar baada ya kufuatilia kwa hatua za awali na kufanya tathmini ya hali ya mambo namna ilivyotokea tarehe 17 juni, 2012 inatoa tamko RASMI kama ifuatavyo: Read the rest of this entry

BREEKING NEWS!!!!! JESHI LA POLISI LAFANYA UNYAMA WA KIHALIFU ZANZIBAR


ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH.

NEWS

LEO TAREHE 17JUN2012 MNAMO MAJIRA YA SAA NANE NANUSU ZA MCHANA TULIONDOKA VIWANJA VYA MALINDI ENEO LA MJINI NA MISAFARA YA MAGARI VESPA NA PIKIPIKI TUKIELEKEA KWENYE MUHADHARA KASKAZINI UNGUJA ENEO LA DONGE KATIKA MSIKITI  UNAOJULIKANA KWA JINA LA DONGE PWANI, TULIPOFIKA MAHONDA MSIKITINI SIOMBALI NA KITUO CHA POLISI CHA MAHONDA MAJIRA YA SAATISA NA ROBO JESHI LA POLISI LILILOVALIA UNIFORM ZA ASKARI WA FFU LIKA-ANZA KURUSHA MABOMU OVYO NA KUANZA KUWATAWANYA WANAOELEKEA KWENYE MUHADHARA DONGE ILI WASIENDELEE NA SAFARI BILA YA KUTOA SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA HIVYO PIA ASKARI HAO HAWAKUTOSHEKA NA KURUSHA MABOMU OVYO PIA LIMEFANYA UNYAMA NA UHALIFU WAHALI YAJUU KWA KU-INAJISI MSIKITI WA IJUMAA WA MAHONDA WALIRUSHA MABOMU YASIOJULIKANA IDADI YAKE NA KUINGIA NDANI YA MSIKITI NA MABUTI NA KUVUNJAVUNJA VYOMBO VILIVYOEGESHWA ENEO LA MSIKITI HUO WA IJUMAA, PIA WALIWAPIGA WANAWAKE WANNE NA MTOTO MMOJA KWA   KUWATIMBA TIMBA BILA YA HURUMA NA KUWAPIGA MARUNGU, ILIPOFIKA WAKATI WA LAASIRI PIA WALIANZA KUPIGA MABOMU NDANI YA MSIKITI WA DONGE PWANI NA WALIKATAKATA KWA VISU MIPIRA YA VESPA NA BAISKELI ZILIZOKUA ZIMEEGESHWA MSIKITINI HAPO NA WALIVUNJA HESHMA YA MSIKITI NA KUINGIA NA MABUTI NDANI YA MSIKITI HUO WALIMKAMATA MZEE MMOJA ALIEKUA AKISWALI SWALA YA LAASIR AMBAE MPAKA SASA HATUJAPATA JINA LAKE, KWA TAARIFA TULIZOZIPATA ZA JUU JUU KUTOKA KWA KAMISHNA WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR WAMEWASWEKA MAHABUSU WATU ISHIRINI………….. INSHA-ALLAH TUNAFUATILIA KWA UKARIBU ………… ANY NEWS TUTAONA KATIKA PAGES ZETU ZINAZOFUATA.


WAHUDUMU WAKISAIDIA WALIOHUDHURIA KWENYE KONGAMANO LA WANAWAKE SKULI YA SEKONDARI HAILE SELASIE