Category Archives: Uncategorized

TANGAZO LA MUHADHARA


BISMILLAH RAHMANI RAHIM

ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH.

JUMUIYA YA UAMSHO INAWATANGAZIA WAISLAMU WOTE WA MJINI NA MASHAMBA MUHADHARA MAALUM UTAKAOFANYIKA MASJID AFRAA KIDONGO CHEKUNDU SIKU YA JUMAPILI TAREHE 09SEP2012 BAADA YA SALA YA LAASIR.

MUHADHIR : AMIR MSELLEM BIN ALLY  NA NAIBU AMIR.

UKIIPATA TAARIFA HII MJUULISHE NA MWENZAKO…….

WABILLAH TAUFIQ

NI MUHIMU KWENDA KUSIKILIZA UJUMBE WA KHERI KWA AJILI YA MASLAHI YAKO YA HAPA DUNIANI NA MAISHA YANAYO KUJA YAANI AKHERA.

Advertisements

WAISLAMU ZANZIBAR TUMESHINDA SENSA IMEFELI ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR


BISMILLAH RAHMANI RAHIM

ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKATUH

WAZANZIBARI TUMESHINDA … SENSA IMEFELI … ALLAH AKUBARIKINI KWA UTIIFU NA UMOJA MLIOUWONESHA.

Namshukuru Allah (s.w).Rehma na amani zimwendee kipenzi chetu Mtume wetu Muhammad (s.a.w) alotuhimiza UMOJA na UTIIFU kwa viongozi na maamuzi wanayokubaliana Waislaam. Allah (s.w) anatuamrisha kwa kusema :

 “..Na shikamaneni enyi waumini na dini na maamrisho yake Allah s.w nyote kwa umoja wenu wala msifarikiane muwe kitu kimoja..) 

Ndugu wakiislaam Allah s.w kama alivotuamrisha kushikamana na kutukataza tusifarikiane vilevile ametukataza tusifanye jambo litakalo tudhoofisha kama kuvutana au kugawana kwa misingi ya kikabila,vyama n.k. kwani mwisho wake ni kumpa nguvu adui yetu na kushindwa.

Allah s.w anatuamrisha kwa kusema: “..wala msivutane mtashindwa na itapotea nguvu yenu..”.

Ndugu zangu nakupongezeni Wazanzibari wote kwa umoja mliouwonesha na UTIIFU kwa viongozi wa umoja wa Jumuiya na Taasisi za kiislaam chini ya Mwevuli wa Jumuiya ya UAMSHO na ndio maana Sensa ikafeli na kulazimika badala ya kufanyika siku moja sasa inafanyika wiki nzima bali inasemekana baada ya kushindwa kupata watu sasa wanarikodi majina ya watoto walopewa vyandarua na waliopigwa shindano za polio pamoja na kutumia vitisho kutoka kwa wakuu wa mikoa, wilaya na jeshi la Polisi, na huwenda wakatumia nguvu na vitisho zaidi kwa siku za mwisho Allah atawashinda kama alivowadhalilisha walipozuwa uongo  kua sh Msellem amehisabiwa pamoja na mimi wakati niko nje ya nchi kwa zaidi ya wiki mbili pia wamejitokeza viongozi wa kisiasa kutaka kuiokoa serikali ya KIKOLONI ya Tanzania ili ifanikishe sensa kwa manufaa ya mkoloni viongozi hao hawakuona haya kuwaambia uongo wananchi hasa pemba kua eti tukiacha kuhesabiwa tutapoteza majimbo wakasahau kua tukifarikiana tutapoteza uhuru wa nchi yetu na sio majimbo tu bali tutabakia kua ni Watumwa wa wakoloni watanganyika kwa Jina la Tanzania.

 Ndugu wa kiislam napenda mfahamu hata kama tutakua wachache basi tukiwa na UMOJA na UTIIFU kwa viongozi tukashikamana na maamrisho hayo kwa uwezo wa Allah TUTASHINDA. Allah anatuambia: 

“..Ni mara nyingi tu kundi dogo hulishinda kundi kubwa kwa Idhni ya Allah naye Allah yuko pamoja na wenye kusubiri..” 

Halkadhalika Mtume s.a.w anatuamrisha UMOJA na kuthibitisha ushindi kutoka kwake s.w kwa kusema: 

“..jilazimisheni UMOJA kwani nusra ya Allah s.w iko pamoja na walioshikamana..”  

NASISITIZA na kukuombeni muyahifadhi maneno haya na kuyakariri kila wakati:

UHURU WA NCHI YETU KWANZA MPAKA TUTOKE KWENYE UKOLONI WA MTANGANYIKA … VYAMA BAADAE Umefika wakati wakuipenda nchi yetu na kuithamini sote kwa umoja wetu tuwe tayari kuvikosa vyama tusikubali kugawanywa kwa misingi ya vyama hizo ni njama za MKOLONI MTANGANYIKA amezitumia na hatoacha kuwatumia vibaraka wake ili wazidi kutugawa na kutubakisha kama watumwa wao na kutudhalilisha wazanzibari na viongozi wetu kwa kichaka cha MUUNGANO wananchi tunadhalilika huku viongozi wakizibwa midomo yao kwa vyeo na nchi yetu inapotea imekua vita vya panzi furaha kwa KUNGURU mkoloni.

Ndugu wazanzibari MUUNGANO NI UKOLONI LAZIMA TUUKATAE NA TUUPIGE VITA KWA NGUVU ZOTE. Tukiwa na umoja TUTASHINDA kwa uwezo wa ALLAH s.w.

                  TUACHIWEEEEE    ………..   TUPUMUWEEEEEEE

 

MSEMAJI  MKUU  WA  UMOJA  WA  JUMUIYA  NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR.

AMIR FARID HADI AHMED.

TANGAZO LA ITIKAFU MASJID AFRAA ZANZIBAR


ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH.

WAISLAMU WOTE KIKE KIUME WA MJINI NA MASHAMBA MNAALIKWA KUHUDHURIA KATIKA ITIKAFU SIKU YA ALHAMIS TAREHE 2AUG2012 ITAKAYO ANZA BAADA YA SWALA YA T ARAWEHE HAPO MASJID AFRAA KIDONGO CHEKUNDU, NIMUHIMU KUFIKA ILI TUKESHE PAMOJA KATIKA KUFANYA DUA YA PAMOJA KATIKA KUIOMBEA DUA NCHI YETU DHIDI YA MAHASIDI WA NDANI NA NJE, ILI ALLAH ATUPE ULINZI NA NUSRA YAKE…..

NIMUHIMU ALIESIKIA TANGAZO HILI AMJUULISHE NA MWENZAKE.

”WABILLAH TAUFIQ”

TUTARUDI TENA KARIBUNI INSHA-ALLAH


ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH.
KUMRADHINI KWA KUWA KIMYA KIPINDI KIREFU… TULIPATA DHARA YA KUHARIBIWA NYEZO ZETU NA JESHI LA POLISI LA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO……!

TAARIFA MAALUM KWA VYOMBO VYA DOLA