WAISLAMU ZANZIBAR TUMESHINDA SENSA IMEFELI ALLAHU AKBAR ALLAHU AKBAR

BISMILLAH RAHMANI RAHIM

ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKATUH

WAZANZIBARI TUMESHINDA … SENSA IMEFELI … ALLAH AKUBARIKINI KWA UTIIFU NA UMOJA MLIOUWONESHA.

Namshukuru Allah (s.w).Rehma na amani zimwendee kipenzi chetu Mtume wetu Muhammad (s.a.w) alotuhimiza UMOJA na UTIIFU kwa viongozi na maamuzi wanayokubaliana Waislaam. Allah (s.w) anatuamrisha kwa kusema :

 “..Na shikamaneni enyi waumini na dini na maamrisho yake Allah s.w nyote kwa umoja wenu wala msifarikiane muwe kitu kimoja..) 

Ndugu wakiislaam Allah s.w kama alivotuamrisha kushikamana na kutukataza tusifarikiane vilevile ametukataza tusifanye jambo litakalo tudhoofisha kama kuvutana au kugawana kwa misingi ya kikabila,vyama n.k. kwani mwisho wake ni kumpa nguvu adui yetu na kushindwa.

Allah s.w anatuamrisha kwa kusema: “..wala msivutane mtashindwa na itapotea nguvu yenu..”.

Ndugu zangu nakupongezeni Wazanzibari wote kwa umoja mliouwonesha na UTIIFU kwa viongozi wa umoja wa Jumuiya na Taasisi za kiislaam chini ya Mwevuli wa Jumuiya ya UAMSHO na ndio maana Sensa ikafeli na kulazimika badala ya kufanyika siku moja sasa inafanyika wiki nzima bali inasemekana baada ya kushindwa kupata watu sasa wanarikodi majina ya watoto walopewa vyandarua na waliopigwa shindano za polio pamoja na kutumia vitisho kutoka kwa wakuu wa mikoa, wilaya na jeshi la Polisi, na huwenda wakatumia nguvu na vitisho zaidi kwa siku za mwisho Allah atawashinda kama alivowadhalilisha walipozuwa uongo  kua sh Msellem amehisabiwa pamoja na mimi wakati niko nje ya nchi kwa zaidi ya wiki mbili pia wamejitokeza viongozi wa kisiasa kutaka kuiokoa serikali ya KIKOLONI ya Tanzania ili ifanikishe sensa kwa manufaa ya mkoloni viongozi hao hawakuona haya kuwaambia uongo wananchi hasa pemba kua eti tukiacha kuhesabiwa tutapoteza majimbo wakasahau kua tukifarikiana tutapoteza uhuru wa nchi yetu na sio majimbo tu bali tutabakia kua ni Watumwa wa wakoloni watanganyika kwa Jina la Tanzania.

 Ndugu wa kiislam napenda mfahamu hata kama tutakua wachache basi tukiwa na UMOJA na UTIIFU kwa viongozi tukashikamana na maamrisho hayo kwa uwezo wa Allah TUTASHINDA. Allah anatuambia: 

“..Ni mara nyingi tu kundi dogo hulishinda kundi kubwa kwa Idhni ya Allah naye Allah yuko pamoja na wenye kusubiri..” 

Halkadhalika Mtume s.a.w anatuamrisha UMOJA na kuthibitisha ushindi kutoka kwake s.w kwa kusema: 

“..jilazimisheni UMOJA kwani nusra ya Allah s.w iko pamoja na walioshikamana..”  

NASISITIZA na kukuombeni muyahifadhi maneno haya na kuyakariri kila wakati:

UHURU WA NCHI YETU KWANZA MPAKA TUTOKE KWENYE UKOLONI WA MTANGANYIKA … VYAMA BAADAE Umefika wakati wakuipenda nchi yetu na kuithamini sote kwa umoja wetu tuwe tayari kuvikosa vyama tusikubali kugawanywa kwa misingi ya vyama hizo ni njama za MKOLONI MTANGANYIKA amezitumia na hatoacha kuwatumia vibaraka wake ili wazidi kutugawa na kutubakisha kama watumwa wao na kutudhalilisha wazanzibari na viongozi wetu kwa kichaka cha MUUNGANO wananchi tunadhalilika huku viongozi wakizibwa midomo yao kwa vyeo na nchi yetu inapotea imekua vita vya panzi furaha kwa KUNGURU mkoloni.

Ndugu wazanzibari MUUNGANO NI UKOLONI LAZIMA TUUKATAE NA TUUPIGE VITA KWA NGUVU ZOTE. Tukiwa na umoja TUTASHINDA kwa uwezo wa ALLAH s.w.

                  TUACHIWEEEEE    ………..   TUPUMUWEEEEEEE

 

MSEMAJI  MKUU  WA  UMOJA  WA  JUMUIYA  NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR.

AMIR FARID HADI AHMED.

Advertisements

About uamshozanzibar

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar

Posted on August 31, 2012, in Uncategorized. Bookmark the permalink. 3 Comments.

  1. waalaykum salaam warahmatullahi wabarakaatuh
    naitwa ibrahim alli kutoka zanzibar meli 4.mimi binafsi naungamkono masheikh wangu wa uamsho na masheikh wengine wote wenye uchungu na uislamu lakini pia wenye uchungu na nchi yetu ya zanzibar.sina uwezo wa mali lakini uwezo alonijaalia mwenyezimungu kunijaalia kujua kuitumia computer na kuwa na e mail na mitandao ya kijamii kama face book twiter n.k nimeona kua kutumia vitu hivi kwa maslahi ya nchi yangu ima kwa kuelwza taarifa ambazo zinapotoshwa,ima kuelezea vipi harakati za jumuiya zinaendelea,laikini pia kutoa elimu kwa wale ambao bado wana mawazo mgando kuhusu muungano,ili wapate wajitambue kua hali halisi sio nzuri ya nchi yetu mpaka sasa, hivyo najitahidi kupinga kwa maneno na hata vitendo muungano huu wa udhalilishaji. na tunashkuru vijana wa uamsho kwenye f book tunafanya kazi nzuri kueneza habari na kutafuta nguvu zaidi ya kuwashinda maadui.
    wabillahi tawfyk.

  2. msimamo ndio huohuo wacha watumie hata vifaru sensa hatuandiki

  3. Asalam alaykum,nawapongeza sana waislam na waumini wote walio gomea SENSA,na Ishallah Muungu yuko pamoja na sisi,na nnawaasa waislam wa zanzibar kuimarisha umoja na mshikamano pamoja na kuzidi kuwatii viongozi wao wa kidini[UAMSHO] Kwamanufaa ya nchi yetu.na tuwetayari kugomea masuala mbalimbali yanayo toka kwa Mkoloni [TANGANYIKA] likiwemo suala la vitambulisho vya mtazania.ASANTEN.MUUNGU ATAWABARIK WOTE WALIO TAYARI KUWATII VIONGOZ WAO.AMIN. By Machano Pandu,Mwanafunzi wa sheria Chuo kikuu cha kiislam Morogoro.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: