Kuhusu Uamsho


Amir Mkuu Jumuiya ya UamshoAssalaam alaykum Warahmatullah Wabarakatuh,

Kila sifa njema inamstahikia Allah (SWT) na rehema na amani zimwendee Mtume Muhammad (SAW) na ahli zake na sahaba wake na waja wema katika Uislam.

Karibu kwenye Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (JUMIKI), jumuiya ambayo imeanzishwa kwa madhumuni ya kuleta mapenzi, umoja na maendeleo miongoni mwa waumini  wa Kiislam; kuendeleza heshima, urithi na historia yao; kuwahamasisha katika masuala ya dini yao, ikiwa ni pamoja na elimu, utamaduni na utukufu wa dini hii kufanya jambo jengine lolote lenye kheri au linalolenga katika kuinua na kuieneza dini ya Kiislam; kulinda na kutetea haki za binaadamu zinazokubalika katika Uislamu ikiwa pamoja  na kumhifadhi Muislamu anapokuwa na shida; kulinda na kutetea silka na utamaduni wa Kiislam usivunjwe, usipotoshwe na usifutwe, na kusaidia kutatua  matatizo yanayotokezea katika jamii ikiwa ni pamoja na migogoro, maafa, na kupambana na majanga mbali mbali ya maradhi kama Ukimwi, matumizi ya madawa ya kulevya na majanga mengine ya kijamii. Soma katiba ya Jumuiya hii hapa…

JUMIKI imesajiliwa rasmi mwaka 2001 na Serikali ya Zanzibar na kupatiwa Namba ya Usajili 149 chini ya Sheria Namba 6 ya mwaka 1995 kuhusiana na Taasisi za Kijamii.