TAARIFA MAALUM KWA VYOMBO VYA DOLA

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI-ZANZIBAR
26/06/2012

TAARIFA MAALUMU KWA VYOMBO VYA DOLA
Kila sifa njema ni zake Allah (S.W.T) mwenye kujuwa siri na dhahiri mjuzi wa yaliyojificha, mwenyekuhudhuria vikao vyote vya uadui na njama za siri na dhahiri hakifichiki kitu au jambo lolote yeye ndie aliesema kwenye kitabu taatifu cha Qur’an “hakuna minong’ono yoyote ya watatu ila yeye huwa wanne, wala ya wanne ila yeye ni watano”. Nae Allah (S.W.T) ndie muweza wa kupindua njama za maadui Allah amesema katika surat Twariq 14-17 “hakika hawa makafiri wanapanga njama na mimi napanga mpango wa kupindua njama zao basi ewe Muhammad wapururie hawa makafiri pole pole mpaka nikuamrishe amri gani kali ya kuwatendea”. hapa pia tunatanguliza dua za utukufu wa daraja kwa Mtume wetu Muhammad (SAW) pamoja na ahli zake na waja wote wema.
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu imelazimika kutoa taarifa hiii maalum kwa vyombo vya dola baada ya kuenea uvumi mkubwa mitaani ya kuwa leo tarehe 26/06/2012 kutakuwa na maandamano na tayari propaganda zinaendelea dhidi ya Jumuiya ya Uamsho, imani yetu na ndivyo inavyosadikika na wengi nchini Zanzibar kuwa propaganda hizo zinaendeshwa na baadhi ya watendaji katika jeshi la polisi na usalama wa taifa baada ya kushindwa kazi zake. Ushahidi wa hayo ni matukio ya tarehe 26-27/06/2012 yaliyotokea hapa nchini kwa chanzo cha ukiukwaji wa jeshi la polisi wa sheria na taratibu za tuhuma, na ubaguzi pamoja na udhalilishaji dhidi ya masheikh walipomkamata sheikh Mussa juma na kumteka kihuni kama majambazi na kukiuka sheria na taratibu zote za uadilifu kwa kumfanya mtuhumiwa ni mhalifu.
Uvunjifu huo na ubaguzi huo umeibua hisia za wanafunzi wa Sheikh Mussa na kuhoji jee! Kuna Padri au askofu yoyote aliepata kudhalilishwa hapa Zanzibar kwa kutuhumiwa? Zaidi ya yote hayo jeshi la polisi limeendelea na kiburi chake wakamnyima dhamana na kuwazuiya jamaa zake na kujenga mazingira mabovu, badala ya kutumia hekima na busara ilitumika nguvu na kuwathibishia wazanzibari kuwa ile ilikuwa agenda maalumu na mpango wa siri kwa wachache kuleta vurugu na kuvunja amani ya nchi iliopo.
Jeshi la polisi walipatiwa taarifa za awali za wahusika wa uchomaji wa makanisa na vile vile JUMIKI imetoa taarifa kwa vyombo vya habari tarehe 03/06/2012, mbali na kukanusha kutohusika na fujo hizo iliitaka serikali kuunda tume na kuwataka vyombo vya usalama vya dola vitoe maelezo sahihi kwa wananchi wa Zanzibar, lakini kwa masikitiko makubwa hakuna taarifa yoyote waliopewa wananchi hadi hii leo zaidi ya kuendesha propaganda na kutoa taarifa za uongo kwa kushirikiana na vyombo vya habari na kusababisha fitna baina ya waumini wa kiisilamu na wakikristo.
Na ushahidi mwengine wa uvunjifu wa amani ni unyama na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanywa na jeshi hilo hilo la polisi na uendelezaji wa ubaguzi nchini Zanzibar dhidi ya raia wa nchi hii,ubaguzi ambao kwa kila mwananchi amejionea mwenyewe, kwani Watanganyika waliofanya maandamano Dar-Es-Salaam juu ya kuwa jeshi la polisi limepiga marufuku maandamano hayo lakini yalifanyika kwa usalama, baada ya siku chache ilishuhudiwa hapa nchini Zanzibar jeshi la polisi kuzuia kwa nguvu zote wananchi wasifike msikitini na kufanya muhadhara wakati haya ndio yaliyokuwa makubaliano baina ya viongozi wa Jumuiya na Kamishna wa jeshi la polisi pamoja na maafisa wa usalama tofauti wa jeshi na serikali zote mbili hapo makao makuu mjini Zanzibar na kuahidi kulipatia utatuzi suala la mihadhara ya nje. Hadi hii leo hakuna utatuzi wowote uliofikiwa zaidi ya ahadi wasizozitimiza.
Jumuiya kwa upande wake imeheshimu makubaliano hayo na ikakubali kujinyima haki yake kwa muda, na ikawa inaendelea na mihadhara misikitini na kuheshimu maamuzi na kuitika wito wa Rais Dkt Shein wa kudumisha na kulinda amani. Lakini kwa masikitiko makubwa jeshi la polisi halikujali chochote wala kuheshimu makubaliano bali lilikuwa likiwapaka matope marais wetu kwa kuvunja amani na haki zote za kibinadamu hatimae 17/06/2012 waliwapiga wananchi eneo la Mahonda, Mkokotoni, Kinyasini na hata wananchi waliopo majumbani huko Donge kwenyewe na ushahidi wa hayo yote upo. Tena tunasema kwa kinywa kipana upo!
Isitoshe walipwapiga mabomu waumini ndani ya sala na walitumia mabomu ya machozi bali pia wametumia mabomu ya moto na kuunguza raia wasiokuwa na hatia nakuunguza mazulia ya msikiti wa mahonda mbali ya kuwadhalilisha wanawake na kuwavua nguo na kuwapiga magongo baada ya kuwakamata mbali ya kejeli na matusi na vibao vya uso, baada ya hapo kuwabambikizia kesi zisizokuwa na mwanzo wala mwisho.
Ili kuthibitisha kuwa walikuwa na agenda maalumu dhidi ya kuzuiya mihadhara, jeshi la polisi linaendelea kushikilia vipasa sauti na mashine zake na gari lililokodiwa kubebea vyombo hivyo na hadi hii leo tokea tarehe 17/06/2012 jeshi la polisi limeshindwa kuwafungulia kesi hata za bandia watendaji hao watatu wa Jumiya walokuwa wakitangaza muhadhara huo uliokuwa ufanyike msikiti wa Donge pwani, awali walitaka kushitakiwa kwa kosa la kutoa matangazo bila ya kibali baada ya siku mbili walibadilishiwa mashtaka na kutaka kupachikwa kesi ya kupiga kelele. Juzi ijumaa walivutana wenyewe wakurugenzi wa mashtaka kurejesha jalada hilo ili watafutiwe kesi nyengine ya bandia kwani kesi hio haikuonekana kuwa inafaa.
Mbali ya usumbufu huo wa gharama ya nenda rudi ya kila siku, hata hiyo gari iliyokodiwa mbali ya kuizuia na kukoseshwa kazi siku zote hizo imevunjwa taa zake za mbele na nyuma hapo hapo kituoni na viongozi wa Jumuiya wameitembelea gari hiyo na kushuhudia mabaki ya vigae vikiwa chini ya gari. Katika vurugu hizo ilizozifanya jeshi la polisi pia hazikusalimika baskeli na vyombo vyengine vya maringi mawili kama vespa kupondwapondwa, kuvunjwa taa, kukatwa mipira kwa visu na hayo yalishuhudiwa na wananchi tofauti wakiwaona hao askari wanaoitwa eti ni wa kuzuia fujo wakifanya uhalifu na unyama wote huo.
Jumuiya ya uamsho baada ya maelezo hayo machache yanayotoa ushahidi wa kutosha juu ya ushiriki wa makusudi wa uanzishaji wa kuvunja amani unaofanywa na jeshi la polisi, Jumuiya imelazimika kutoa taarifa hii hadharani kuwa haijaandaa maandamano leo hii na wala haijatangaza. Ni imani yetu viongozi wa Jumuiya kuwa propaganda hizi za kuwepo maandamano leo ni mtiririko wa agenda zao za siri wasioitakia mema nchi yetu ya Zanzibar yenye malengo ya kuitia hatiani Jumuiya na kuipaka matope sambamba na kuwashitaki viongozi wakiwa na lengo la kukusudia kuzima harakati za vugu vugu la wananchi kudai Zanzibar yao ijitawale na kuhakikisha kuwa Rais wetu mpenzi Dkt Shein anatambulika kitaifa na kimataifa na kurejeshewa heshima yake kikamilifu ya kukalia kiti chake cha umoja wa mataifa na kuhakikisha serikali yetu ya umoja wa kitaifa inatoka katika mikono ya utumwa na ukoloni wa Watanganyika nakuwa huru kwenye maamuzi ya nchi na maendeleo ya taifa, pamoja na kuwasaidia wananchi kutokana na udhalili wa umasikini uliodumu kwa miaka 48 na kupata uhuru wa kutumia rasilimali zake bila ya kuhojiwa na wakoloni wasioitakia mema nchi yetu Zanzibar.

Jumuiya inapenda kuhitimisha taarifa hii kwa taarifa MUHIMU SANA iliowasili hivi punde tu juu ya kukamilika mkakati wa muda mrefu wa kutaka kuwabatiza viongozi wakuu wa jumuiya kesi za ugaidi hususan Amir Mkuu wa jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed. Inasemekana kua kuna mahusiano makubwa baina ya watendaji ndani ya Jeshi la polisi na usalama pamoja nabaadhi ya wageni wanaosadikiwa kuwa ni raia wa Marekani juu ya kuutekeleza mkakati huo baada ya kuwa tayari umeshakamilika.

WABILLAH TAUFIQ
ALLAH MTUKUFU NDIE MLINZI WETU
Imesainiwa na

………………………………..
Naibu Amir Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya Kiisilam

NAKALA:
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Makamu wa Rais wa kwanza
Makamu wa Rais wa Pili
Waziri wa Katiba na Sheria
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Inspector General Police
Kamishna wa Jeshi la polisi Zanzibar
Ofisi ya Umoja wa Mataifa Zanzibar
Mabalozi wote nchini
Vyombo vya habari
Waislamu wote Tanzania

Posted on June 26, 2012, in Uncategorized. Bookmark the permalink. 5 Comments.

  1. PONGEZA ZA KUTOSHA KWA VIONGOZ WOTE WA UAMSHO KWA KUANDIKA BARUA HII,BARUA HII NI MWIBA WA KOO KWA MAFISAD NA MADHWALIM

  2. Tunaamini kuepo kwa agenda za siri lkn Allah ndie alotufungulia njia kuptia Jumuiya yetu na YEYE atapindua hila zao makafiri hawa

  3. Kama allah ameshasema niombeni nami nitakujibuni basi hayo yote tunamwachia yeye nj kwa uwezo wake zanzibar itasimama si kwa magongo.inshaallah

  4. Mohamed S Suleiman

    Assalaamu alaykum warahmatu llah.Cna mengi ya kuongea ilanawatakia kwa allah dua na inshaallah Zanzuibar huru tutaipata lakini ustahamilivu ndio dira ya mafanikio yetu tusichoke wala tuckate tamaa na nyinyi viongozi wetu mucrudi nyuma.IKO CKU ITAKUWA NI HISTORIA KAMA ILIVYO HISTORIA YA FATHU MAKKA

Leave a comment