MSIMAMO WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISILAMU ZANZIBAR JUU YA MCHAKATO WA KATIBA

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI-ZANZIBAR
24/06/2012

Bismillahir Rahmaanir Rahiim
Kila sifa njema zinamstahikia Allah (S.W.T), rehema na amani zimuendee Mtume wake, ahli zake na wafuasi wake wote waliomfuata kwa wema. Baada ya vikao tofauti vya uongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Zanzibar, zimeonelea kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki katika mchakato wa kutoa maoni kuhusu katiba mpya kwa sababu kuu zifuatazo:
1. Vikao vyote vya uongozi vilikataa katakata suala zima la kususia na ilikubalika azimio la kuwa tusitoe mwanya kwa maadui zetu wasioitakia mema nchi yetu Zanzibar wakutusemea na kutoa maoni dhidi ya nchi yetu ya Zanzibar.
2. Kushiriki kwetu tunatengeneza hoja ya vitendo na kuzidi kuuthibitishia ulimwengu na serikali yetu ya umoja wa kitaifa chini ya uongozi imara wa Rais wetu mpenzi Dkt Ali Muhammed Shein kuwa Jumuiya za Kiisilamu hazina nia mbaya wala hazijapata kuwa na nia mbaya ya kuleta vurugu au kuvunja amani kama lilivyofanya jeshi la polisi tarehe 17/06/2012 huko Mahonda, Donge, Mkokotoni na maeneo mengine pamoja na kunajisi msikiti na kuharibu mali ya misikiti ikiwemo kuunguza mazulia ya msikiti wa Mahonda. Pia kuwapiga mabomu ya moto waumini wasio na silaha ndani ya sala na kuwadhalilisha wanawake kwa kuwavua nguo na kuwajeruhi vibaya sana.
3. Kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Shein katika suala la umoja ni nguvu na kutotoa mwanya kivitendo wa kuwagawa wananchi wa Zanzibar, kwani Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisilamu kwa muda wote baada ya kukabidhiwa na Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu kazi ya kuelimisha UMMAH wa kizanzibari kupitia mihadhara ilikuwa ikisisitiza kwa nguvu zote umuhimu wa umoja. Imani yetu sisi viongozi kuwa “KWA UMOJA WETU TUTASHINDA”.
4. Kushiriki kwetu kutaweka rekodi sahihi na halisi ya wazanzibari ndani ya tume ya kupokea maoni juu ya mchakato wa katiba mpya ili kuipa fursa tume hiyo na hasa wakurugenzi kutoka Zanzibar pamoja na wabunge na wawakilishi katika Bunge la katiba kuitetea nchi yetu Zanzibar na kumrejeshea Rais wetu heshima ya kutambulika kimataifa na kuifanya nchi yetu iwe na mamlaka kamili ya kujiamulia kwa uhuru bila ya kuingiliwa.
5. Kutumia fursa hii ya mchakato wa katiba mpya kuimarisha muungano wa kijamii na kuondoa dhulma ya muungano wa kiserikali ulioidhulumu nchi yetu kiunyama haki zake za kimataifa na hata za kitaifa na kufikia hadi kuifuta nchi yetu ya Zanzibar katika ramani ya dunia.
6. Tamko la wazi la mwenyekiti wa tume ya ukusanyaji wa maoni kuhusiana na katiba mpya Mh. Jaji Warioba alilolitoa mbele ya waandishi wa habari alipoizindua tume hiyo mjini Dar-Es-Salaam siku ya Jumatatu 18/06/2012 kwamba maoni yoyote yataheshimika na kuzingatiwa ikiwemo suala zima la muungano pamoja na yale maoni ya watu wanaoukataa muungano. Lakini bado wazanzibari tunawasiwasi mkubwa sana.
Kutokana na sababu zilizotangulia kutajwa hapo juu na baada ya mashauriano na viongozi tofauti katika jamii, Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu ndiyo imetoa uwamuzi wa kuwataka waumini na wazanzibari wote kushiriki katika kutoa maoni lakini sambamba na uwamuzi huo.

Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu, unapenda utoe tanbihi na tahadhari ya hali ya juu kwa tume na kuitaka ifanye kazi yake kwa uadilifu. Kwani uongozi pamoja na wazanzibari wengi kutokana na udanganyifu wa tume zote zilizotangulia za uchaguzi, bado wasi wasi mkubwa umetanda pamoja na imani ya kuwa haki haitotendeka.

 

Vile vile tunawasiwasi mkubwa wa mamlaka za nchi kupitia watu wachache wenye lengo la kufanikisha maslahi yao binafsi, wataingilia utendaji wa tume na shughuli zake kiutendaji kwa kuiburuza katika malengo binafsi na kwa hilo hapa sisi viongozi wa umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu tunatamka wazi kwamba hazitonyamaza kwa udanganyifu na dhulma yoyote itakayofanyika na haitamstahamiliya wala kumuonea haya kiongozi yoyote kwa dhulma hiyo.
Pia umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu, zinatoa wito kwa wazanzibari wote pamoja na viongozi wa kisiasa kuungana na wazanzibari wote na kutumia fursa hii ya mabadiliko ya katiba kudai Zanzibar yetu huru. Kauli mbiu yetu iwe…
“…TUNATAKA NCHI YETU ZANZIBAR NA TUNATAKA MAMLAKA KAMILI YA ZANZIBAR…”.
Sambamba na hili, tunaomba viongozi wetu wa kisiasa wasiwaingize wazanzibari katika MTEGO wa watanganyika wachache wanaotaka kuidhulumu Zanzibar kwa kuwatamkisha wafuasi wa CCM kukariri maoni ya kutaka serikali mbili sambamba na kuwatamkisha wafuasi wa CUF maoni ya serikali mbili na mkataba ili isemwe mwisho wa rekodi za tume kuwa wazanzibari wanataka serikali mbili na kulitupia mbali neno la mkataba hatimae ni kubakishwa serikali zilizopo kama zilivyo na muungano wa dhulma dhidi ya Zanzibar uliodumu kwa muda wa nusu karne na kuwatia wazanzibari katika kitanzi cha nusu karne nyengine.
Tunawatahadharisha wazanzibari tusiingie katika mtego huo, TUUNGANE sote kwa kauli moja TUNATAKA HESHMA YA RAIS WETU, TUNATAKA HESHMI YA NCHI YETU, TUNATAKA HESHMA NA MAMLAKA KAMILI YA NCHI YETU. Huu si wakati wa kunadi sera za vyama tukifanya hivyo lazima tutajigawa na kuwapa nguvu maadui zetu, umoja wetu ndiyo silaha yetu. Tupaze sauti zetu kwa sera ya uzalendo:
“…TUNATAKA NCHI YETU YENYE MAMLAKA KAMILI (FULL SOVEREIGNITY)…”
Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu unapenda kuwathibitishia waislamu na wazanzibari wote kwa ujumla wao kuwa tupo palepale katika lengo kuu la kuitaka nchi yetu Zanzibar kwa gharama yoyote ile na bado tutaendelea kudai nchi yetu mpaka tone la mwisho la uhai wetu. Tunawataka wazanzibari wote sambamba na kujitokeza kwa wingi kutoa maoni ,tuendelee kwa wingi zaidi katika kuorodhesha majina yetu kwa umoja wetu sote katika fomu maalumu iliyoandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu kukusanya majina ya wazanzibari wanaodai haki yao ya kikatiba ya “KURA YA MAONI” kuhusu Zanzibar na muungano, Jee! Wanautaka au hawautaki? Haki hii ya kudai kura ya maoni imo ndani ya katiba yetu ya Zanzibar ibara ya (80A). Kwa haki hiyo HATUNA MJADALA, tusiogope kauli za Wakuu wa Mikoa wanaopotosha wananchi kwa silaha ya vitisho wakiwa wanayakini na kutambua kua hawana haki hiyo. Wazanzibari hiyo ni haki yetu ya kikatiba na tutaendelea kuidai kwa amani MPAKA TUIPATE ZANZIBAR YETU HURU YENYE MAMLAKA KAMILI.
Serikali zote duniani, mara nyingi zinalinda malengo yake kwa mtutu na vitisho lakini kwa upande wa wananchi mara nyingi sana matakwa yao hubezwa na kutupiliwa mbali, hivyo kwa kuzingatia hayo hatuna budi kujenga ngome imara, na kwa mantiki hiyo tunaanza safari yetu kwa kuweka ulinzi imara baada ya kumtegema Allah (S.W.T) kuunganisha nguvu yetu na kujipima kiutendaji.

Allah amejaalia nguvu yetu ni katika umoja wetu kivitendo lengo la azimio letu hili ni kuhakikisha tunatoa shindikizo la kutosha ili haki itendeke, kwa maana hiyo basi tunatangaza rasmi kwamba tunawaunga mkono waislamu wenzetu wa Tanganyika katika suala zima la kuikataa sensa ya taifa. Mbali na sababu zao za msingi, kwa upande wa Zanzibar tunasababu ya msingi na ndio kipaumbele chetu, si jengine ila ni nchi yetu na tunatamka wazi kwamba, HATUTOSHIRIKI SENSA MPAKA TUIPATE NCHI YETU KWANZA.

 

“…ZANZIBAR HURU IKO NJIANI… UMOJA WETU NDIO SILAHA YETU…”
WABILLAH TAUFIQ
…………………
Sheikh, Farid Hadi Ahmed
0777421813
MSEMAJI MKUU WA UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISILAMU ZANZIBAR

 

NAKALA:
Mh. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Mh. Katibu Mkuu CUF
Mh. Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar
Ofisi ya Umoja wa Mataifa Zanzibar
Mabalozi wote nchini
Vyombo vya habari
Waislamu wote Tanzania

Advertisements

About uamshozanzibar

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar

Posted on June 24, 2012, in Uncategorized. Bookmark the permalink. 5 Comments.

 1. Kwanza kabisa, naipongeza JUMIKI kwa taratibu nzuri za kisheria ktk kila hatua ya harakati za maendeleo juu ya mustakbali wa nchi yetu ya ZNZ na wazanzibari kwa ujumla.
  Lakin lapili, kweli siku ya Jumatat, tarehe 18/06/2012 Jaji Warrioba akizungumza na waandishi wa habari nchini, jijini Dares- es-salam, alisema suala la kusikilizwa maoni ya watu wote hata wale wanaopinga muungano, Jee tuna imani kiasi gani na kauli yake hii wakati tunamjua yy ni mtanganyika na ni ktk walewale wanaopiga msuak asubuhi na jioni kwa lengo la kuitafuna kiurahisi ZNZ yetu. Mm kama mzanzibari nina wasiwasi sana na kauli yake hii.
  Mwisho kabisa, jicho letu wazanzibari tumeshalitoa kwenye uwanja wa wanasiasa na tumelielekeza kwenye Jumuiya zetu za kiislam kwa kujua kwamba ktk siasa tulijsahau na sasa tumekumbuka, sambamba na hilo, nawaomba viongozi wetu mjuwe kuwa zaid ya watu 95% waliopo ZNZ na nje ya ZNZ wanaiunga mkono JUMIKI juu ya hatma ya znz yetu. mm naaihid kutoa ushirikiano wa hali zote, naomba umakini wenu.
  AHSANTE SANA.

 2. JAMANI UAMSHO MUPO AU NDO NA NYIE MSATISHWA WAZANZIBAR TUMEAPA KUA MKITUGEUKA KWANZA TWAANZA NYIE NDIO TUNAT………..

  • uamshozanzibar

   ASSLAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH.

   SH. biidhnillah mpaka kieleweke au ALLAH aturuzuku shahada…….

   JE wewe ukotayari kwa haya………?

 3. UAMSHO TUMEJIPANGA VIPI NA KUPOKEA MATOKEO BAADA YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA MPYA

  • uamshozanzibar

   ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH.

   Shukran, kwa suali lako.

   Matokeo ya mchakato wa katiba tunafahamu kwamba yatakwenda kinyume na maoni yatakayo tolewa na WaZanzibari hili lipo katika historia tokea zilipoundwa tume za kukusanya maoni haijawahi kutokea maoni ya Rai ya kasikilizwa, Fuatilia Tume ya Jaji Rorbert Kisanga na Pia tume Ya Jaji nyalali.

   Zingatia kwamba mchakato wa katiba sio njia yetu ya kuipata Zanzibar Huru, Bado tupo katika mchakato wa kuitafuta Zanzibar yetu huru mpaka KITAKAPO ELEWEKA INSHA-ALLAH njia ya kisheria ni kwa kupitia kura ya MAONI.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: