Monthly Archives: May 2009

Katiba ya Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam


logoKATIBA YA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAM

UTANGULIZI

Pale ambapo hapana umoja miongoni mwa Waislam;

Na pale ambapo hapana kusaidiana miongoni mwa Waislam;

Na pale ambapo maasi yameenea katika jamii;

Na pale ambapo maadili mema yamepote;

IPO HAJA ya kuunda Jumuiya itakayowakumbusha waislam kufanya mema na kuacha maovu;

Jumuiya ambayo itawaunganisha Waislam na kurejesha heshima ya Uislam;

Jumuiya ambayo itawakutanisha waislam katika juhudi zao za pamoja kurudisha utukufu wa Uislam. Read the rest of this entry

Advertisements

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh


Wapendwa Ndugu Waislam na Watembeleaji wote wa Weblog hii,

Shukrani zote njema zinamstahikia Allah (SWT), Mungu wa Kweli na wa Haki, Bwana wa Mbingu na Ardhi na Mlezi wa Walimwengu wote. Rehema na amani ziwe juu ya Mtume wake Muhammad (SAW), mjumbe aliyetumwa kwa walimwengu wa mataifa yote kuunasihi umma kufuata njia iliyonyooka, yaani Uislam.

Hili ni jaribio la kwanza la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar, kuwasiliana na ulimwengu kupitia njia hii ya mawasiliano ya kisasa. Tunawakaribisha nyote katika uwanja huu mpana wa mawasiliano. Kwa kuwa ndio kwanza weblog hii imo kwenye matayarisho, tunahitaji msaada wa mawazo na maoni ya namna bora ya kuiendesha kutoka kwenu.

Karibuni sana!