Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh

Wapendwa Ndugu Waislam na Watembeleaji wote wa Weblog hii,

Shukrani zote njema zinamstahikia Allah (SWT), Mungu wa Kweli na wa Haki, Bwana wa Mbingu na Ardhi na Mlezi wa Walimwengu wote. Rehema na amani ziwe juu ya Mtume wake Muhammad (SAW), mjumbe aliyetumwa kwa walimwengu wa mataifa yote kuunasihi umma kufuata njia iliyonyooka, yaani Uislam.

Hili ni jaribio la kwanza la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar, kuwasiliana na ulimwengu kupitia njia hii ya mawasiliano ya kisasa. Tunawakaribisha nyote katika uwanja huu mpana wa mawasiliano. Kwa kuwa ndio kwanza weblog hii imo kwenye matayarisho, tunahitaji msaada wa mawazo na maoni ya namna bora ya kuiendesha kutoka kwenu.

Karibuni sana!

Advertisements

About uamshozanzibar

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar

Posted on May 4, 2009, in Uncategorized. Bookmark the permalink. 4 Comments.

 1. Seif azan al rawahy

  Am asalam alaykum.napenda kui2mia fursa hii kutoa contribution yangu kama ifuatavyo: 1.website inahitaji m2 maalum kwa ajili ya kuiongoza hapa namaanisha moderator.huyu majukumu yake ni kuweka sawa na ku up date taarifa ndani ya wakati.namaanisha ni lazima pawepo m2 makhsusi kwa ajili ya ku up load habar na documantation zote ndani ya website. 2.hivyo ili hilo lifanikiwe mnahitaji muwe creative na mu-brainstorm kwa ajili ya kufikia lengo la kuwafikia jamii ya kiislam na kutoa ushawishi na elimu kwa umma kupitia network yenu. 3.binafsi nipo katika maandalizi ya kukamilisha website ye2 ya Dar es alaam ambayo ni ya ki2o cha utafiti cha kiislam (islamic center for research) lengo ni kutafsiri vitabu kutoka lugha za kigeni kwenda lugha ya kiswahili,kufanya utafiti na kutoa takwimu juu mas ala yanayohusu uislam na waislam..kama islamic website itakuwa ni information centre. So ni vizuri mkaiga mfumo wetu. Soon itakapokuwa tayari 2tawajulisha. Ahsanteni.

 2. Asalam Alaykum, hii Jumuiya imekuja katika wakati muafaka na inapohitajika hasa, hutafuti suluhisho ikiwa hapana matatizo, hutungi sheria iwapo hakuna sheria inayovunjwa lakini kila linaloboreshwa limeporomoka na ndiyo maana likaboreshwa.
  Zanzibar hatusemi hata tupo katika njia panda , kwani iwapo upo kwenye njia panda unaweza kurudi nyuma kidogo ukatoka kwenye kipanda cha njia halafu ukaaanza kutafuta njia yako, leo sisi tumeanza kupotea, kupoteza, njia imeota nyasi, maadili yamekufa, mzee tayari amekua mtoto, washirikina katika serikali yetu kwa kufuata mifumo ya kikafiri inayotuchanganya , inawanufaisha wale waliokubali mifumo hiyo yenye taathira mbaya kesho mbele ya haki, uchumi umeporomoka kiajabu kuna kila kitu katika masoko yetu, ingia mwanakwerekwe kuna matunda ambayo tulikua hatujawahi kuyaona siku za nyumba lakini ni wangapi wanakula matunda hayo, kipande cha samaki kinaanza shilingi elfu mbili na nusu , mshahara wa mtu mwenye familia ya mke na watoto sita kama unafika laki mbili kwa mwezi kabahatika mwezi unasiku kwa uchache ni siku ishirini na nane , familia hii mapembe inakula kwa uchache kilo moja na nusu uliza bei ya pembe hilo, huyu hawazi kuigusa ndizi sokoni ya kula watu wanane, hii laki mbili ilikua anywe chai tu, jee kweli tunaishi katika uhalali kwa njia hizi? jee kweli tutanyamaza hapa bila yakujadili muunano huu ambao unambana muuzaji huyu kwa kodi za mauzo za TRA(teteresha, Rarua na Angusha ) “ili wasije juu”. tukija kwenye utamaduni na maadili, viongozi wetu wahayaoni hayo inawezekana wamo kwenye magagari yenye vioo vya kiza, vivazi wanavyovaa wenzetu watoto wameiga, vifuko vya viroba vimo chochoroni mwa nyumba watoto wadogo wanaokota na kufyonza mabaki na wengine wako mashule wameanza kujua bangi, unga, ulevi, lugha zao kwa wazee wanajua wenyewe, jee hizi ndizo haki za binaadamu, tunahitaji muungano uvunjike tufanye kazi ya kurejesha hadhi ya nchi hii, watoto wanatutoka tutakwenda kujibu, binafsi mimi nashindwa sasa, ni vigumu kudhibiti wakati nje hakuna udhibiti, na hizi ni haki za binaadamu za muungano ambazo zimeanzia mbali, tutafikisha pabaya mno, maberedhuli leo wanajifaharisha, wanajumuiya tayari na inajulikana wanaitwa kwenye mikutano na kulipwa hutoka Pemba wakalipiwa nauli kujakuimarisha, laiti kama tungekua na mamlaka ya kupanga uamuzi basi tungejua ni jinsi gani tupange uchumi wetu, hatuhitaji mafuta Zanzibar tunahiji mipango tu, vijana wasengepiga debe wanane gari moja ,kazi zipo ni mipango kwa sababu mpaka upangiwe, Muungano una malengo na inaonyesha wameyafikia 60% lakini tunaweza kuyafuta yote hayo nakuijenga Zanzibar

 3. Assalamualaykum , nawapongeza sana ktk harakati zenu mbalimbali za kijamii ikiwemo kuutanabahisha umma wa kiislam juu ya hali ya uislam zanzibar.Kuna masuala kadha wa kadha ambayo mm binafc cjapendezwa nayo imma kwa kuckia kutoka kwa watu mbalimbali haswa vijana.Swala la kuuvunja muungano limepokelewa na watu wengi kama njia sahihi ya kuinasua jamii ya wazanzibari kuondokana na kuburuzwa na serikali kuu ya muungano.Shaka yangu ni “misconception” ya lengo kuu la kutaka kuuvunja muungano.Watu wengi hawajafahamu tafcri haswa ya kusudio lenyewe nackia tu watanganyika wende kwao tuacheni tupumue n.k.
  Kuna haja ya kutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusu lengo lenu kwa umma wa kizanzibari ili icje kuwa munawatenganisha badala ya kuwaunganisha.Pia matumizi ya “strong words” yaliyosheheni jazba na hamasa yana hatari kwa amani na utulivu ktk vicwa vya zanzibar.Nina maelezo mengi ya kufafanua nia yangu lakini kwa leo INSHALLAH naishia hapa nitaendelea iwapo nitajibiwa.
  Wabillahitawfiq

  • Maneno yako ni mazima, lakini nadhani kufikia lengo la kuelewesha juu ya malengo ya muungano ni kwamba kunahitajika nyanja nyengine za kueneza elimu hii ni wachache wanapata fursa ya kuingia kwenye blog, mfano leo kuna muhadhara kutokana na ugonjwa wa muda mrefu wa mtoto wangu nimedharurika, kwa hivyo si sote tunasikia mihadhara inayofunua vichwa lakini na vijarida vinahitajika

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: