Katiba ya Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam

logoKATIBA YA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAM

UTANGULIZI

Pale ambapo hapana umoja miongoni mwa Waislam;

Na pale ambapo hapana kusaidiana miongoni mwa Waislam;

Na pale ambapo maasi yameenea katika jamii;

Na pale ambapo maadili mema yamepote;

IPO HAJA ya kuunda Jumuiya itakayowakumbusha waislam kufanya mema na kuacha maovu;

Jumuiya ambayo itawaunganisha Waislam na kurejesha heshima ya Uislam;

Jumuiya ambayo itawakutanisha waislam katika juhudi zao za pamoja kurudisha utukufu wa Uislam.

SEHEMU YA KWANZA
1. JINA

Jumuiya hii inayoanzishwa kwa mujibu wa Katiba hii itaitwa
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAM au kwa
Lugha ya Kiingereza “THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION” kwa ufupi AIMP.

2. HADHI

Jumuiya itakuwa ni chombo huru kinachojitegemea na kwa jina
Lake wenyewe kuweza kumiliki mali pamoja na kuwa na uwezo
Wa kushtaki ama kushatakiwa.

3. LUGHA

Katika utendaji wa shughuli zake. Jumuiya itatumia lugha ya
Kiswahili na Kiingereza au lugha yoyote nyengine itakayihitajika.

4. MAKAO MAKUU

Makao makuu ya Jumuiya yatakuwa katika Mji wa Zanzibar.
Jumuiya inaweza pia kufungua watawi katika sehemu kadhaa
za Unguja na Pemba kufuatana na mahitajio.

SEHEMU YA PILI

5. MADHUMUNI

AIMP inaanza ikiwa na madhumuni yafuatayo:-

(a) Kuleta mapenzi, umoja na maendeleo miongoni mwa waumini wa
Kiislam;

(b) Kuendeleza heshima, urithi na historia ya kiislam;

(c) Kuwahamasisha waislam katika masuala ya dini yao
Ikiwa ni pamoja na elimu, utamaduni na utukufu wa dini
Ya kiislam;

(d) Kufanya jambo jengine lolote lenye kheri au linalolenga
Katika kuinua na kuieneza dini ya kiislam;

(e) Kulinda na kutetea haki za Binaadamu zinazokubalika katika Uislamu ikiwa pamoja na kumhifadhi muislamu anapokuwa na shida;
(f) Kulinda na kutetea silka na utamaduni wa kiislamu (usivunjwe,usipotoshwe,usifutwe,).

(g.) kusaidia kutatua matatizo yanayotokezea katika jamii ikiwa ni
pamoja na migogoro, maafa ,na kupambana na majanga mbali mbali ya . maradhi kama ukimwi, matumizi ya madawa ya kulevya nk.

6. NJIA ZA UFANIKISHAJI

Katika kufikia madhumuni yaliyoolezwa katika ibara
Iliyotangulia, AIMP inakusudia kufanya yafuatayo:-

(a) Kuwakutanisha waislam katika mihadhara, ibada za
za pamoja na shughuli nyengine za dini;

(b) Kuratibu masuala ua elimu ya uamsho kupitia:-

(i) Mihadhara , madarasa.

(ii) Kuandika vitabu na makala majarida na magazeti kuhusiana na mada mbali mbali.

(iii) Kufanya ziara, semina, warsha na mijadala.

( c ) AIMP itatafuta mawasiliano ya karibu na waislam au
vikundi vya kiislam vya ndani na nje ya nchi kwa jili ya
kuimarisha mapenzi, umoja na mshikamano miongoni
mwa waislam.

(d) Kuhamasisha kuishi katika utamaduni wa kiislam kwa
maneno na vitendo.

(g) Jumuiya itahusisha na kujenga hisani na mazingira
Bora;

(h) AIMP itafanya au kusaidia kufanywa shughuli yoyote
Yenye lengo la kuendeleza uislam na waislam.pamoja na kuunda kamati za utendaji katika kufanisha malengo na madhumuni hayo.

SEHEMU YA TATU

7. UANACHAMA

(a) Kila muislam mwenye umri usiopungua miaka 18 na
Ambae anakubali kuitii katiba hii, anaweza kuwa
Mwanachana wa AIMP.

(b) Maombi ya uanachama yatafanywa kwa kujaza fomu
Maalum itakayowekwa kwa ajili hiyo.

( c ) Kila mwanachama atakuwa na haki zifuatazo:-

(i) Kulingana na masharti yaliyowekwa na katiba hii,
Kushuriki na kutoa maamuzi katika shughuli zote
Za Jumuiya.

(ii) Kuchagua ama kuchaguliwa kushika nafasi yoyote
Ya uongonzi.

(iii) Wakati wowote atakapoona muafaka, kutoka Katika Jumuiya kwa amani na usalam

( d ) Kila mwanachama atakuwa na wajibu kama ifuatavyo:-

(iv) Kulipa ada maalum ya kiingilio katika Jumuiya.
Ada hii haitorudishwa kwa mwanchama endapo
Ataacha kuwa mwanachama au katika hali
Nyengine yoyote.

(v) Kulipa ada ya kila mwaka kama itakavyowekwa na
Kamati kuu.

(vi) Kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za
Jumuiya ambazo zina muhusu.

(vii) Kutekeleza majukumu yoyote mengine kama
atakavyopangiwa na uongozi wa Jumuiya.

(e) Mwanachana atapoteza sifa za uanachama endapo
Moja au zaidi ya haya yafuatayo litatokea:-

( i ) Iwapo atafariki

(ii) Kwa hiari yake, atakapoacha uanachama;

(iii). Endapo utafukuzwa uanachama na kamati kuu;

SEHEMU YA NNE

8. UTAMADUNI WA AIMP

(a) AIMP itakuwa na utamaduni wa kiislam uliyojengeka
Kutokana na Quran na Sunna za Mtume (SAW);

(b) Jumuiya haitokuwa na dhahebu maalum bali mwanachama
Wanaweza kuwa ni waislam wa madhehebu tofauti;

( c ) Jumuiya itakuwa na utamaduni wa kutatua migogoro
ya waislam kwa hekma na ustarabu mkubwa.

( d ) Jumuiya haitakuwa na uhusiano wowote na chama chochote cha siasa.

SEHEMU YA TANO

9. VYOMBO VYA KIUTAWALA

Jumuiya itakuwa na vyombo vya utawala vifuatavyo:-

(a) Mkutano Mkuu.

(b) Bodi ya Wadhamini.

(c) Kamati Kuu.

A. MKUTANO MKUU

(a) Mkutano Mkuu utajumuisha wanachama wote wa AIMP na
Utaitishwa angalau mara kwa mwaka au kukiwa na dharura ya kuitisha mkutano mkuu. Mkutano Mkuu utakuwa ndio chombo cha juu kabisa katika
Jumuiya.

(b) Mkutano Mkuu utaongozwa na Amir ambae pia atakuwa
Ndie mlezi wa Jumuiya.

( c ) Mkutano Mkuu utakuwa na majukumu yafuatayo:-

(i) Kuchagua Amir na naibu Amiri, Mshika Fedha na
Wajumbe wote wa bodi ya Wadhamini na Kamati Kuu.

(ii) Kupokea na kupitisha au kujadili ripoti za utekelezaji kama
Zitavyowasilishwa na Kamati Kuu;

(iii) Kupitia na kupitisha au kuacha kupitisha bajeti ya
Ya Jumuiya kwa mwaka ujao wa fedha.

(iv) Kupokea na kujadili ripoti ya mapato na matumizi kwa
Mwaka wa fedha uliopita;

(v) Kurekebisha Katiba endapo wazo la kufanya hivyo
Litawasilishwa na Kamati Kuu na kukubaliwa na
Wanachama wasiopungua theluthi mbili ya
Wanachama wote;

(vi) Kufanya jambo jengine lolote linalohitajika kwa
Mujibu wa sheria ya Jumuiya ya 1995, Katiba hii
Au sheria nyengine ya nchi kuhusiana na Jumuiya.

B. BODI YA WADHAMINI

(a) Bodi ya Wadhamini itakuwa ni chombo cha pili katika
Uongozi wa Jumuiya.

(b) Bodi itakuwa na wajumbe wasiopungua watano na
Wasiozidi kumi watakaoteuliwa ma Kutano Mkuu kutoka
Miongoni mwa waislam;

( c ) Mwenyekiti wa Bodi atachaguliwa na mkutano mkuu
na ni yeye atakaeongoza mikutano yote ya Bodi. Endapo
Mwenyekiti atakuwa hayupo basi Bodi
itamteua mmoja miongoni mwao ili kuchukua nafasi ya
mwenyekiti kwa madhumuni ya kikao au vikao hivyo.

(d) Bodi itakutana angalau mara nne kwa mwaka.

(d) Bodi ndiyo itashirikiana na Kamati kuu itakuwa ndiyo mlinzi
na msimamizi mkuu wa Jumuiya na mali zake zote. Na kwa
nafasi hiyo Bodi ndiyo itakayokuwa na uwezo, kwa niaba ya
Jumuiya, kushtaki ama kushtakiwa, kumiliki, kuuza na kununua
Mali ilimradi tu iwe kwa maslahi ya waislam.

(f) Bodi ndiyo itakayokuwa na mamlaka ya kutoa ufafanuzi
kuhusiana na vifungu vya Katiba hii.

(i) Endapo kutatokea matatizo yoyote ndani ya Jumuiya
Basi Bodi ndiyo itakayofanya kazi ya usuluhishi.

(i) Bodi inaweza kuanzisha kamati ndogo ndogo kwa
madhumuni ya kushughulikia suala lolote la Jumuiya .
Uongozi na utaratibu wa kazi wa kamati hizo pia
utapangwa na Bodi.

C. KAMATI KUU

(a) Kutakuwa na Kamati Kuu ya Jumuiya ambayo itakuwa
Ndiyo dhamana wa shughuli za kila siku za Jumuiya,
Wajumbe wote wa Kamati Kuu watakuwa wanaishi
Zanzibar.

(b) Kamati Kuu itakuwa na Amiri, Katibu Mkuu, Mshika fedha
Na wajumbe wengine kumi;

( c ) Kamati Kuu itakutana chini ya Amiri angalau mara moja
kwa mwezi.

(d) Masuala yote ya uajiri, uachishaji au ufukuzaji kazi
yatakuwa chini ya Kamati Kuu.

(e) Ili kuweka ufanisi kazini, Kamati Kuu inaweza kuunda
vitengo au idara mbali mbali na kuwateua viongozi wa
vitengo au idara hizo.

(f) Kamati Kuu inaweza kuweka kanuni na taratibu ambazo
itabidi zifuatwe na wanchama na viongozi wote wa
Jumuiya. Isipokuwa kwamba kanuni na taratibu hizo
Lazima zisithibitishwe na Bodi ya Wadhamini kabla y a
Kuanza kutumika kwa mujibu wa katiba.

(g) Kamati Kuu itakuwa na jukumu la kutayarisha programu
ya utekelezaji wa shughuli za Jumuiya kwa mwaka
mzima.

(h) kamati kuu itahakikisha kwamba malengo ya Jumuiya yalioelezwa katika katiba hii yanafikiwa.

SEHEMU YA SITA

10. VIONGOZI WA JUMUIYA

AIMP itakuwa na viongozi wafuatao:-

(a) Amir;
(b) Naibu Amir;

(c) Katibu Mkuu;
(d) Naibu katibu mkuu;

(e) Mshika Fedha;

(f) Wajumbe.

A. AMIRI

(a) Amiri atakuwa kiongozi mkuu wa Jumuiya na
Atachaguliwa kwa wingi wa kura katika Mkutano Mkuu wa
Jumuiya. Isipokuwa kwamba Amiri wa mwanzo wa
Jumuiya atateuliwa na wanachama waanzilishi na atashika nafasi hiyo hadi hapo Mkutano Mkuu
Utakapoamua kuchagua Amiri mwengine.

(b) Amiri alichaguliwa hushiuka awadhifa huo atabaki kwa
Kipindi cha miaka 3 na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi chengune cha miaka 3.

( c ) Amiri ataitisha na kusimamia vikao vyote vya Mkutano
Mkuu, na Kamati Kuu.

(d ) Amir anaweza kuondoshwa madarakani kwa azimio
Litakapopitishwa katika Kamati Kuu na kuungwa mkono
Na theluthi mbili ya wajumbe wote wa Kamati Kuu.

B. KATIBU MKUU

(a) Kutakuwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ambaye pia
Atakuwa ndiye katibu wa Bodi na Kamati Kuu. Jumuiya
Inaweza pia kuweka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu pindipo
Itaona ipo haja ya kufanya hivyo.

(b) Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, kadri itakavyokuwa,
watachanguliwa na Bodi ya Wadhamini katika kikao maalum kilichoitishwa kwa ajili hiyo na wataendelea kushika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 3 na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi chengine cha miaka 3 na si zaidi.

( c ) Katika kupitisha maamuzi yoyote yanayohitajika kupigiwa
kura, Katibu Mkuu hatoruhusiwa kupiga kura.

(d) Katibu Mkuu na Naibu wake (kama yupo) watakuwa na
majukumu yafuatayo:-

a Kwa mashirikiano na Amiri, kuuitisha vikao vyote
vya Mkutano Mkuu, Bodi na Kamati Kuu.

b Kupanga ajenda zitakazozungumza katika vikao hivyo.

c Kuweka kumbukumbu zote za Jumuiya.

d. Kuweka vyema daftari la wanachama wote wa jumuiya . pamoja na kuwaingiza wale wapya wanaojiunga na kuwafuta wale ambao, kwa sababu yoyote, wamesita kuwa wanachama.

e. Kufanya shughuli za kila siku za Jumuiya.

f. Kufanya jambo jengine lolote kama atakavyoamriwa
na Amir au Bodi au Kamati Kuu.

g. Iwapo Katibu mkuu au Naibu itathibitishwa kwamba wamefanya
Jambo lolote ambalo ni kinyume cha maadili ya Jumuiya au cha aibu au kuvunja Katiba hii basi Bodi itakuwa na mamlaka ya
Kusimamisha uongozi.uamuzi wa ama kumfukuza au kumrudisha
Kazini utapitishwa na Mkutano Mkuu wa Jumuiya.

C. MSHIKA FEDHA

(a) Kutakuwa na Mshika Fedha wa AIMP ambae
Atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Jumuiya.

(b) Mshima Fedha atashika wadhifa huo kwa kipindi cha
Miaka mitatu lakini anaweza kuchaguliwa kushika tena
Nafasi hiyo kwa kipindi cha pili cha miaka mitatu.

( c ) Mshika Fedha atakuwa ndio dhamana na msimamizi wa
fedha zote za Jumuiya.

(d) Mshika fedha atafungua akauti moja au zaid katika
Benki ya Watu wa Zanzibar au benki nyengine ziliopo
Nchini kama ambavyo Kamati Kuu itaelekeza.

(e) Mshika Fedha ataweka kumbukumbu zote za mapato na
matumizi ya Jumuiya na atakuwa na wajibu kila ifikapo
mwisho wa mwaka wa fedha wa Jumuiya, kufunga
hesabu za Jumuiya.

(f) Kamati Kuu inaweza endapo itaona muafaka, kuajiri au
Kuomba, kwa makubaliano maalum, huduma za mkaguzi
wa hesabu ili kuchungua hesabu za Jumuiya.

(g) Kamati Kuu inaweza kuweka nafasi na kumteua
Msaidizi Mshika Fedha ili kumsaidia Mshika Fedha pale
Atakapokuwa na haja ya kufanya hivyo.

(h) Endapo Mshika Fedha au msaidizi wake (kama yupo)
atakwenda kinyume na maadili, au atavunja masharti ya
Katiba hii au kufanya kitendo chochote chenye kuleta
aibu kwa Jumuiya, basi Bodi ya Wadhamini inaweza
Kumsimamisha kazi na endapo haitoridhika na utetezi
Wake, basi itamfukuza kabisa.

Isipokuwa kwamba Mshika Fedha aliyefukuzwa kazi kama
hakuridhika na uamuzi wa Bodi basi anaweza kupeleka rufaa
yake katika kikao cha Mkutano Mkuu ambao baada ya
kusikiliza pande zote itatoa uamuzi kufuatana na wingi wa kura.

D. WAJUMBE

(a) Wajumbe wote wa bodi ya Wadhamini na kamati Kuu
Waliochaguliwa kwa mujibu wa Katiba hii nao watakuwa ni
Viongozi wa Jumuiya hii ya AIMP

(b) Wajumbe watashika nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitatu na
wanaweza kuendelea kutumikia Jumuiya pindipo
watachaguliwa tena .Hakutokuwa na kikomo cha utumishi wa
Mjumbe katika Bodi au kamati Kuu.

( c ) Mjumbe yoyote anaweza kuondolewa madarakani kwa azimio
lililopitishwa na kuungwa mkono na theluthi mbili au zaidi ya
wajumbe wa bodi ya wadhamini ikiwa mjumbe huyo amefanya
kitendo au jambo lolote ambalo ni kinyume na maadili ya
Jumuiya au cha aibu au kuvunja katiba hii, Isipokuwa
ieleweke wazi kwamba hakuna mtu atakaehukumuwa bila ya
Kwanza kupewa nafasi ya kujitetea.

(c) Iwapo mjumbe aliyeondoshwa madarakani hakuridhika na
Uamuzi wa Bodi, basi anaweza kupeleka rufaa yake katika kikao cha mkutano Mkuu ambapo uamuzi wake utakuwa ni wa
Mwisho.

12. MIKUTANO

(a) Katika mkutano au kikao chochote cha Jumuiya, basi nusu ya
Wajumbe wa mkutano au kikao hicho itatosha kuendelea na mkutano
au kikao hicho, katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya,
Iwapo nusu ya wajumbe haikupatikana basi theluthi moja ya
Wajumbe wote itatosha kuendelea na Mkutano siku nyengine ambapo mkutano huo utaitishwa.

(b) Uamuzi wowote katika Mkutano Mkuu au vikao vyengine vya
AIMP utafikiwa kutokana na wingi wa kura isipokuwa labla
Wajumbe wawe wamewafikiana wote kwa jumla. Katika upigaji kura za ndio na siyo basi Amir atakuwa na kura ya ziada baada
Ya ile kura yake ya kawaida.

( c ) Katibu Mkuu au kama itakavyokuwa, Msaidizi wake ataweka
kumbukumbu zote za viako. Kumbukumbu hizo zitathibitishwa
au vyenginevyo katika kiao kitakachofuata cha kamati husika
au Mkutano Mkuu.

12. UWAJIBIKAJI

(a) Mamlaka yote ya AIMP yatakuwa mikononi mwa wanachama na hivyo basi viongozi wa Jumuiya watawajibika moja kwa moja
kwa wanachama waliowaweka madarakani.

(b) Wanachama nao watakuwa na wajibu wa kutoa ushirikiano wa
kweli kwa viongozi wa Jumuiya ili kufanya kazi ya uongozi iwe
nyepesi.

( c ) Itakuwa ni wajibu wa viongozi na wanachama kufanya shughuli
zao kwa mujibu wa maelekezo ya Quran, Sunna na Katiba hii.

13. MASUALA YA FEDHA

(a) Fedha za Jumuiya zitatokana na vianzio
Vifuatavyo:-

(i) Ada za kujiunga na Jumuiya;

(ii) Michango ya wanachama;

(iii) Misaada na ruzuku kwa wahisani wa ndani na nje
Ya nchi;

(iv) Mauzo ya kanda, hotuba na vijitabu mbali mbali
Vitakavyotolewa na masheikh kuhusu mada tofauti.

(b) Fedha za Jumuiya zitatumika kwa madhumuni ya kuendeleza
Malengo ya Jumuiya.

(c) Viongozi wote wa Jumuiya hawatolipwa mshahara. Isipokuwa
Kwamba Jumuiya, kama hali itaruhusu, inaweza ikatoa posho la safari na vikao. Isipokuwa vile vile, Jumuiya itarudisha
Gharama za halali alizoingia Kiongozi au mwanachama yoyote,
Kutokana na kufanya shughuli za Jumuiya.

(d) Katika kuidhinisha matumizi yoyote basi itabidi kupatikane saini
Mbili kati ya viongozi wa juu yaani Amir, Katibu Mkuu na Mshika fedha.

14. MAHUSIANO

AIMP itaanisha kuendeleza mahusiano mazuri na watu binafsi, taasisi
za Serikali, mashirika, makampuni na taasisi binafsi yoyote ya ndani na nje ya
Nchi ilimradi tu mtu au vyombo hivyo viwe na malengo yanayoendana
na malengo ya Jumuiya.

15. NEMBO

(a) AIMP itakuwa na alama maalum ya utambulisho kama ambavyo
Itakubaliwa na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Jumuiya
Kutokana na mapendekezo ya kamati kuu.

(b) Nembo ya Jumuiya itatumika katika mawasiliano yote ya
Jumuiya itakuwa chini ya kabidhi ya Katibu Mkuu.

16. KUVUNJWA KWA AIMP

(a) Jumuiya ya AIMP inaweza kuvunjwa wakati wowote baada ya
Kikao cha dharura cha Mkutano Mkuu kilichoitishwa kwa ajili
Hiyo kupitisha kwa robo tatu ya wajumbe wote, azimio la
Kuivunja Jumuiya.

(b) Endapo Jumuiya itavujwa basi mali na madeni yake yote
(kama yapo) zitahamishiwa kwa Jumuiya nyengine yenye
malengo yanayofanana na yale ya AIMP iliyovunjwa.

17. MAREKEBISHO

(a) Katiba hii inaweza kurekebishwa au kufutwa na kuandikwa upya
iwapo azimio la namna hiyo litakubaliwa na theluthi mbili au
zaidi ya wajumbe wote wa Mkutano Mkuu.

(c) Mabadiliko yoyote yatayotokea ni lazima yawasilishwe kwa
Mrajis wa Jumuiya kabla ya kuanza kutumika.

18. MASUALA YA MPITO

(a) Mpaka wakati ambapo Mkutano Mkuu wa kwanza wa Jumuiya
Utakapoitishwa kwa mujibu wa katiba hii, wale viongozi
waanzishi wataendelea kufanya shughuli za Jumuiya kama
kwamba wamechaguliwa kihalali kwa mujibu wa masharti ya
katiba hii.

(b) Jambo lolote lililofanywa au litakalofanywa na viongozi hao
Waanzilishi litahesabiwa kama kwamba limefanywa na viongozi
Wa Jumuiya waliochaguliwa kisheria.

19. KUANZA KUTUMIKA.

Katiba hii itaanza kutumika mara tu baada ya kupata usajili.

لجنة الدعوة الإسلامية

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU

THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION

ZANZIBAR

Advertisements

About uamshozanzibar

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar

Posted on May 20, 2009, in Uncategorized. Bookmark the permalink. 7 Comments.

 1. RAMAZANI MUSSA

  asalam alaykoum
  mimi ni mkaaji wa R D congo nintakuombeni msaada wa fikra ya maendeleo ya dini yatu wiisalm kwani huku kwetu kuna wa kristu wengi paseta 99% ninatarajia kama fikra zangu mutaziunga mkono ili janga la ukristo tupate kuupunguza hapa kwetu .malala miko haya ni ushahidi mbele ya ALLAH .MSITUACHE KATIKA UPOTEVU .WENU NDUGU
  RAMAZANI MUSSA
  TEL:+243997047629
  +243853535232
  UVIRA/RD CONGO

 2. tushikamane na dini ya kiislamu

 3. tunaomba tuwekeeni formu za kusign kuhusu kura ya maoni wengine tuko nje tutajaza then tutawatumieni baada ya kuscan. Tunavyo vitambulisho vya uraia pia

 4. tupo pamoja inshaallah na jumuiya yetu Allah atuongoze

 5. uamsho for muslims, for humanity

 6. MAONI YANGU MM KWA JUMUIA NI, NAONA MAAMIRI SASA TUNATAKUANZA KUOGOPA KATIKA HARAKATI ZA KUPIGANIA NCHI YETU; TUNATAKA KUSHIRIKI KATIKA KUTOA MAONI,
  LAKINI HATUONI KUA PANA MTEGO WAMETUTEGA AWA,
  HIVI NANI KATI YETU HAJUII KAMA KATIBA YAO MPYA WASHAINDAA?
  TUNAFIKIRIA KWELI WATAWEZA KUBADILI MUELEKEO WAO HAWA?

 7. Abdulrahim Said (Liirahim)

  kila la kheri katika kuimarisha Uislamu duniania
  mola azidi kuturahisishia
  amiin

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: