‘Siasa bila dini ni uendawazimu’ – Kanisa

Sheikh Farid Hadi wa Uamsho

Imetumwa na Abdul Shani katika mtandao wa Zanzinet:

Katika kusoma soma habari kwenye Jamii Forums, kuna mtu alituma hii. Hebu na tuangalia Wakristo wanavyoambiana kuhusu kuchanganya dini na siasa.

Na Lilian Nyenza

Kanisa halitaacha kutoa mwongozo kwa watu wake hata kwa mambo ya kisiasa ukiwamo uchaguzi kwa kuwa, siasa bila dini ni sawa na uendawazimu.
Aidha, imedaiwa kuwa tabia ya kuwalaghai vijana kuwa ni taifa la kesho, ndiyo inayowadumaza kiakili na kuwafanya watumiwe na wanasiasa kufanya fujo, badala ya kujitokeza kuongoza kwa kufuata taratibu za nchi.

Mkurugenzi wa chama cha kifamilia cha Undugu Association Tanzania, Padri Baptiste Mapunda, alitoa kauli hiyo katika sherehe za kuuaga mwaka 2004 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2005, zilizofanyika katika ukumbi wa Parokia ya Mt. Yosefu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo wa UNDUGU ASSOCIATION TANZANIA alisema kuwa, Tanzania imeanza kuonesha dalili mbaya za machafuko kutokana na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa kuweka mbele ubinafsi.

“Tukikaa kimya huku mambo yanaharibika katika jamii; eti tuwaachie wanasiasa wafanye watakavyo, tutakuwa hatutendi wajibu wetu na hivyo, Kanisa halitaacha kusema ukweli kwa maslahi ya umma hata kama unamkera mtu. Hii ni kwa kuwa tunajua wazi kuwa siasa bila dini, ni uendawazimu ambao mtu hajui akifanyacho kwa kuwa akili yake haijatimia kiroho.” alisema.

Aliitaka jamiii ya Kitanzania ijifunze thamani ya amani na siasa safi kutokana na hali ya amani na usalama katika nchi jirani za Rwanda na Burundi ambayo ni hatari na inasikitisha.

Alisema vita na mauaji yanayoendelea katika nchi hizo, yanasababishwa na uroho wa madaraka wa watu wachache ambao hawajali utu wa wengine.
Aliongeza kuwa, “Siku zote tunapaswa kukumbuka kuwa, amani na mapendo ambayo Mungu ametujalia, tunapaswa kuyaenzi sisi sote kwa kuwa siasa bila dini, ni sawa na uendawazimu.”

Padri Mapunda aliiasa jamii kuendelea kumuomba Mungu ili azidi kuwajalia amani,upendo na utulivu uliopo sasa, kuwa uwepo hata baada ya Uchaguzi Mkuu kupita.
Amewataka Waamini kuwaombea viongozi wanyanyasaji kama Herode, wabadilike na hivyo, kuongoza nchi kwa haki na akawasihi Watanzania kuyashinda maovu kwa kutenda yaliyo mema.

Hata hivyo, Padri Mapunda amewatahadharisha vijana kujiepusha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa siasa, kwa nia ya kufanya fujo katika uchaguzi.
“Vijana mara nyingi wamekuwa wepesi wa kurubuniwa na vijizawadi vidogo vidogo, ili wafanye kile wanachokitaka wanasiasa wabinafsi. Sasa mimi nasema mkae chini na mlitafakari hilo kwa makini. Mtakao angamia ni ninyi na si wao,” alitahadharisha.

Alisema vijana ni Taifa la leo na Taifa bila vijana limekufa, hivyo aliwasihi kuwaheshimu wazazi na walezi ili wapate kuishi maisha marefu na yenye heri duniani, kama walivyojaliwa kuuona mwaka huu mpya.

Naye Mwenyekiti wa Umoja huo, Bw. Benjamini Komba alisema, lengo la Shirika la Undugu, ni kuiunganisha jamii, ikiwa ni pamoja na kuimarisha Ukristo katika kupata hamasa katika kazi ya umisionari, ili ijengeke roho ya umisionari wa kweli nchini Tanzania.

Bw. Komba alisema kuwa, Shirika limekuwa na mchango mkubwa kwa jamii, kwa kuwa ni chombo cha kuelimisha jamii na kuendeleza mawasiliano na wamisionari wa Afrika ambao wapo ndani na nje ya nchi kwa lengo la kusukuma mbele kurudumu la Injili katika Taifa hili.
Umoja huo haujishughulishi na mambo ya siasa na hauna ubaguzi wa dini, rangi, imani wala itikadi.
Katika sherehe hizo, Wanaundugu na watu wengine walialikwa na kuhudhuria pamoja na familia zao.

Advertisements

About uamshozanzibar

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar

Posted on June 11, 2012, in Uncategorized. Bookmark the permalink. 1 Comment.

  1. WAKRISTO, MSITUZUNGUKE AKILI, SISI TUNAJUA KWAMBA WIMBO WA TAIFA NI WIMBO WA KANISA, Rejea kitabu cha nyimbo na sala cha kanisa katoliki), PIA, TUNAJUA MWENGE NI ZAO LA FIKRA ZA KANISA.Rejea kalenda ya mwenge itolewayo na kanisa). HIVYO DINI INAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUFINYANAGA WANAJAMII, WAISLAMAU WAKIFANYA WAO KOSA. KUNA NINI KWA WAO?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: