“Nape, waombe radhi Uamsho na Wazanzibari”

Haya ndiyo madai halali ya Wazanzibari.

Barua hii imetumwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook leo (10 Juni 2012), nasi tumeichapa kama ilivyo.

Wakati nikisikiliza uchambuzi wa magazeti, asubuhi hii ya leo, nilishtushwa sana na kicha cha habari kisemacho ‘ CCM yafananisha Uamsho na Majambazi’ sikutaka kuamini kwa haraka,nikataka nijionee mwenyewe, ni gazeti gani liloandika hivyo, ndio nikaelewa kuwa ni gazeti la Nipashe la Jumapili, tarehe 10-16 toleo namba 057410.

Kauli hii ilitolewa na Katibu wa itikadi, Siasa na Uenezi, Muheshiwa Nape Nnauye. Nilipoona kuali hii, hapa nanukuu..”…Uamsho ni majambazi, na kwa kuwa serikali hii ni ya CCM, tunataka iwashuhulikie kama inavyofanya kwa majambazi wengine bila ya kuwaangalia sura,”mwisho wa kunukuu,Gazeti ka Majira 10-16 Juni,2012 ndio nikakubali kuwa nilichokisikia ni sahihi.

Awali ya yote, pamoja na kauli hiyo siamini kabisa kwamba kauli ile ni ya Chama Changu cha CCM, hata kidogo siamini hilo. Kama suala ni vurugu, lilojumuisha kuchowa nyumba za ibada ikiwemo makanisa na msikiti,mabaa na magasti . kwa nadhani kila mtu amelilaani na kwa sababu kuna vyombo maalum ya kushuhulikia masuala haya, basi vyombo hivyo viachiwe vifanye kazi zake.

Sasa inakuwaje Mhe. Nape anachukulia mamlaka ya kuchunguza na kutoa hukumu kwamba ‘Uamsho’ ndio walifanya yale, kama hivyo ndio, sidhani kuwa kungekuwa na haja ya kuanzishwa jeshi la polisi na Mahakama, badala yake Muheshimiwa Nape, pekee angetosha kufanya kazi hiyo.

Lakini la pili, namsihi ngugu yangu Nape, uombe radhi kwa waislamu kwa kuwatusi na kuwadhalilisha, ‘Uamsho’ ni taasisi iliosajiliwa kisheria kwa malengo mahusisi yanayotafsiriwa kutoka na Qur an na Sunna- hata hivyo Sina uhakika kuwa, Muheshimiwa Nape anafahamu kuwa uislamu si kuswali na kusoma maulidi tu…lakini hili sipaha pake, – sasa unaposema Uamsho ni kama majambazi unakusudia kuwa mafundisho ya vitabu vyao ni ujambazi na wafuazi wake ni majambazi kule Zanzibar?

Lakini la tatu, Hivi ndugu yangu Nape, hawa walioisajili taasisi hii, walikuwa mataahira? Kwa kutokuona kuwa ‘Uamsho’ ni kama genge la majambazi? Hii inaleta taswira kuwa serikali ya Zanzibar haiku makini au nayo ni sehemu ya magenge ya ujambazi ndio maana wakaisajili na kuruhusu ‘Uamsho’ kufanya kazi zake huko Zanzibar, kwa hili nalo nakuomba uwaombe radhi wazanzibar haraka sana.

Kwa sababu sitaki kuamini kuwa kauli ile ni ya chama changu makini, CCM, Mimi nadhani, ndugu yangu Nape, umekwenda mbali mno, hayo ni matusi makubwa sana kwetu, nadhani huna taarifa sahii za ‘Uamsho’ na wala hutaki kuelewa hilo, lakini kama kijana, ambaye nakuona potential na unaonesha Positive Thinking, nakusihi Uombe radhi – hilo ni jambo la kiungwana sana .

Advertisements

About uamshozanzibar

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar

Posted on June 10, 2012, in Uncategorized. Bookmark the permalink. 4 Comments.

 1. Nape uombe radhi

 2. KWELI ZANZIBAR INADHARAULIWA YAANI HATA MWENYEKITI QWA CHAMA ANAWEZA KUITUKANA TAASISI HALALI ILIYOPEWA ZAMANA YA KUSAJILI TAASISI YA KASHFIWA NA YO PIA IMEKAA KIMYA? HE?

  • uamshozanzibar

   ASSALAMU ALAYKU WARAHMATULLAH WABARAKATUH.
   Sh. haya hatokezea endapo tu haijui mipaka yake!!!! na kujisahau kwa kibri cha ulua aliokua nao…
   Kwa upande wetu haturudi nyuma.

   >WABILLAHI TAUFIQ<

 3. Wana njama tu hao, asitubabaishe.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: