“NI kweli Uamsho wamo serikalini” – Jibu la Vjana wa Uamsho kwa Wassira na UVCCM

Na Sujae Mkiji


Jana tulisikia kauli zenu na mukasema Uamsho wapo Serikali. Sisi tunayakubali maneno yenu na tunakiri kuwa ni kweli Uamsho wapo Serikalini. Ila nyinyi mumeshindwa kuwataja kwa majina sisi tutawataja kwa majina na vyeo vyao. Muamsho wa kwanza ni Rais Jakaya Kikwete. Yeye ametuamsha kwa kutwambia wazi Wazanzibari kuwa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba haitoratibu Muungano. Hivyo ametuamsha na kutuwekea bayana Wazanzibari kuwa Tume hiyo haituhusu, sisi Wazanzibar kinachotuhusu kwenye Katiba ni Muungano. Katuamsha kuwa Tume hii ya Katiba si ya Muungano.

Kikwete huyo huyo ametwambia kuwa Muungano ushavunjwa na CCM NEC, na alisema NEC imeshaamuwa kuwa Rais wa Zanzibar asiwe Makamu wa Rais wa Muungano. Hivyo ametuamsha kuwa NEC imeenda kivyume na Hati ya Muungano na kwenda kivyume na makubaliano ni kuyavunja makubaliano, hivyo NEC imeuvunja Muungano.

Muamsho mkubwa zaidi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Yeye alituamsha pakubwa tena akatutowa kwenye usingizi mzito pale alipotwambia kuwa Zanzibar si Nchi. Hata alipoambiwa ni nchi amekosea, akasema: “Sijakosea wala sijalewa. Zanzibar si nchi.” Kwa hakika, Pinda ametuamsha pakubwa.

Muamsho mwengine ni Mwalimu Julius Nyerere alipotwambia amechoka na sisi Wazanzibari; na hapa namnukuu: “Tumechoshwa na Wazanzibar i na Uislaam.” Kama si Muamsho, huyu ni nani?

Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Marehemu Mzee wetu Abeid Amani Karume, alituachia uswiya kwamba “Muungano ni kama koti, likitubana tutalivuwa!” Naye pia ni Muamsho.

Muamsho mwengine ni Mansour Yussuf Himid. Naye katuamsha si haba pale aliposema ndani ya Baraza la Wawakilishi kuwa serikali moja hataki kuisikia, mbili ni butu, anataka serikali tatu au vyenginevyo.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita, Shujaa Amani Karume ndiye aliyezidi sio tu kutuamsha, bali pia akatuletea Umoja wa Kitaifa na Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya mwaka 2010 tena akaifanya iwe shoka la kuvunja Muungano. Isomeni vizuri Katiba ya Zanzibar na hapo mutajuwa kuwa Karume ni Muamsho au si Muamsho.

Kwa hiyo, Stephen Wassira na UVCCM hamjakosea kusema Muamsho wapo Serikalini. Ni kweli. Tena wapo serikali ya Chama chenu. Wala msimtafute mchawi. Wachawi wenyenu.

Advertisements

About uamshozanzibar

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, Zanzibar

Posted on June 6, 2012, in Uncategorized. Bookmark the permalink. 3 Comments.

 1. Nadhani watakuwa wanaanza kufahamu,kuwa dhulma ya Tanganyika ndiyo inayotuamsha.
  Pia viongozi wao ambao walishindwa kujizuia kuropokwa na kuonesha dhamira mbaya kwa Dola ya Zanzibar pia ilichangia kiasi kikubwa kutuamsha.
  Vitendo vya mauwaji ya wananchi wasiokuwa na hatia nyakati mbalimbali katika visiwa vya Unguja na Pemba pia nikatika vitu vinavyoendelea kutuamsha.
  Maasi yanayofanywa na vikosi vya Tanganyika bila ya kupelekwa katika vyombo vya sheria nikatika sababu zilizotufanya kuomba uhuru wa nchi yetu!Kwasababu mtu asiepata haki katika nchi yake inamaanisha kuwa hayuko huru.

 2. SADAKTA.
  Uzi ni ule ule, mpaka kitaeleweka.

  Zanzibar huru kwanza!

 3. Kadri siku zinavoenda mbele, uamsho inazdi kupata wajumbe kadhaa wa kadha kutoka serikalini wanaingia ktk uamsho. Naomba leo nikutajieni wajumbe wapya ambao pengine awali walikua wanachama wa uamsho kimya kimya lakn sasa rasmi wamejidhihirisha.
  Kwanza ni huyu babu yetu Ruksa, ameamua kuingia ktk kazi ya kuwaamsha wazanzibari kwa maksud pale aliposema kuwa uamsho ni sawa na ALQAYDA, BOKO HARAM nk, jambo ambalo lilimpelekea Sh Farid, viongozi wote wa jumuiya na wazanzibari wote kwa ujumla kuongeza nguvu zao ktk harakat za ukomboz wa ZNZ.
  Mashallah, akina mama nao hawako nyuma hata kidogo, kwani bint Suluhu naye pia kajtangaza waziwazi kufanya kazi za uamsho majukwaani pale alipoona wanafunzi wa vyuo vikuu wamelala kuhusiana na suala zima la muungano. Nashkur mm bnafsi niliamka na kauli zake hizo alipohutubia Mahfali ya wanafunz Morogoro hususan pale aliposema kuwa wazanzibari tunashangaza kusema hatuoni faida za muungano, au hatuna macho, aliyasema haya akiwa na hoja yake kubwa eti urojo sasa unauzwa huku Tanganyika. Kwa kweli wengi wetu tuliamka na tukaamini kwamba “ADUI WA MTI SI SHOKA, NI MTI WENYEWE”
  Kwa leo nimekutajieni hao tu, nawasihi wasomaji wa blog hii unganeni nasi kwa kadri watu wanavojiunga na Uamsho tutakujuvyeni Insha’allah.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: